Tuesday, January 13, 2015

MAREJEO-WIZI WA KAZI YETU TOKA TAWI LA DODOMA TANZANIA-BIORN PRODUCTION Mwaka jana mnamo mwezi wa september Uongozi wa studios za biornproduction zote zilitangaza rasmi kuwa Hawafanyi kazi tena na aliyekuwa msanii wa label aitwaye One Six toka pande za Central Zone Dodoma. Kifupi si msanii wetu tena. Tukazuia nyimbo zake tatu (3) kati ya nne alizokuwa na project nazo kwetu. Tukiacha Maya ambayo ameshafanyiwa video chini ya Kampuni ya Afterday light Films,Chini ya Director Erick-Backamaza. Moja kati ya nyimbo 3 zilizozuiwa imeibwa na kuwekwa kwenye mitandao mbali mbali na inaendelea kuwa downloaded kwa maelezo ya kwamba imepatikana toka Kifimbo fm dodoma. Uongozi wa Biornproduction Studios unalaani na kupiga marufuku wimbo huo kutumiwa na yeyote mahala popote kwa matumizi ya aina yeyote sababu ni Mali ya studio Kwa mujibu wa sheria na taratibu za kampuni ya Biorn zinavyoelekeza. Hatua kali za kisheria na kibinadamu zitatumika kulinda haki yetu kama watayarishaji wa kazi hii popote tutakapo baini muhusika wa wizi huu.


No comments:

Post a Comment