Saturday, February 21, 2015

It's hard to explain how we feel it's a painful n' sad moment may god rest his soul in eternal peace. Biorn Production Studios inakutakia pumziko lenye kheri M/mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Background History # Life before death with Biorn Production. Kwa mara ya kwanza nilimjua na tulimpokea kwa mara ya kwanza tukiwa tunaishi maeneo ya kurasini,temeke Dar es salaam mwanzoni mwa mwaka 1999. Alipata kampani kubwa sana,kipindi hicho cha mapinduzi ya kukua na kuchipukia kwa mziki wa bongo flavour. Tayari kurasini au tmk yetu ilishakuwa na wasanii pia makundi ambayo yana nguvu km Kiroboto (Juma Nature),Maffia Mobb,Manduli Mobb,Stara Thomas,Watwist,Kundi kubwa la RnB la kina J4 linaitwa Akili Tribe na ndiyo kundi ambalo marehemu aliimbia kwa kukaribishwa na Steve ambaye ndiye alikuwa kiongozi. Katika harakati za mziki nikafanikiwa kumjua zaidi Mez B mnamo mwaka 2002 kwani tulikuwa na mizunguko ya kila siku kikazi kwenye studio za master j, yeye na jamaa zake wa Akili Tribe kwa ajili ya project zao. Bila kusahau kundi la baba yako hapa Premier Gangstarz (PG). Siku zilipoenda nikajikita kwenye Mziki zaidi na ndipo nilipokutana na ndugu yangu Moog. Ambaye kwa ushirikiano nae tukafanikiwa kufungua studio ya kurekodi mziki Biorn record mwaka 2005,Maeneo ya mabibo hostel ubungo,Dar es salaam. Tangu hapo tukazidi kuwa karibu na marehemu Mez B na mwaka 2006 tukafanikiwa kurekodi nae bonge la wimbo uliitwa 'Wacha Niende' sweet RnB ikasumbua sana radios stations. Ujamaa ukazidi na akatuletea marafiki zaiki kama K Bazili,G solo toka dodoma,Ngwair etc. Na ndipo tulipokuja kukutana na vikwazo ikatulazimu kubadili jina Studio yetu na kuiita Kama Kawa-Record then tukapiga kazi na Ngwair Speed 120 kwenye corner shaa, Mapacha,Danny Msimamo akafanyiwa remix ya wimbo Mic chini ya Proffesor Ludigo & Wagosi wa kaya na wengine wengi lakini ulifika muda tukaamua kupumzika na production hivyo kumuuzia studio G solo na familia yake ikiwemo kuwakabidhi pia Producer Marijani. Danny X na Moog tukageukia mlango mwengine wa maisha yetu mpaka mwaka 2014 tulipoamua kuirudisha tena studio yetu Biorn Production safari hii ikiwa East Zoo maili mbili Dodoma...Opposite na oysterbay bar. Tumshukuru Mungu kwa kila jambo,kwani still tuliobakia pia ni marehemu watarajiwa zaidi napata nguvu kuona still bado tupo na baadhi ya waanzilishi wa wanachemba pia bado Biorn inakabidhiwa wanachemba wapya wenye kasi kama waliyokuwa nayo waanzilishi na wanafanya kazi nzuri kina Big Born90. Poleni sana kina Darkmaster,One six-Victor,Noorah na wengineo wote kwani msiba ni wetu sote. R.I.P. Mez B.


No comments:

Post a Comment