Katika hali ya kukata ukimya wa kutofanya recording kwa kipindi kirefu kufuatia maboresho ya Jengo la Studio za Biorn Production tawi la Dodoma,mkurugenzi mtendaji bwana Muharami. Omary. Ngwila.(Moo G.) Ameweka bayana sababu zilizopelekea hali hiyo kupitia studio za radio ras fm 100.5 alipoongozana na wana biorn Dash-Touches ambaye ni producer mahiri anaekuja kwa kasi ya hatari kwa kupika ngoma nyingi kali na msanii Big born 90 anaesumbua na wimbo wa Raggae ya Mama Africa uliyotaarishwa na Producer huyo kisha kufanyiwa Video kali na Muandaaji Moe Kaali toka Studio za One4pixel jijini Dodoma.
Mkurugenzi Moo G. Amebainisha kwamba kulingana na mahitaji na changamoto zinazoikabili kanda ya kati na mikoa ya jirani uongozi mzima wa Biorn umeona kuna kila haja ya kuongeza wigo wa kutoa huduma kwa kuongeza baadhi ya vipengele ambavyo vitarahisisha ufanyaji wa kazi za sanaa kwenye kanda hiyo kulingana na kasi ya ukuaji wa mziki nchini na dunia kwa ujumla.
Hivyo walilazimika kusitisha huduma za kurekodi ili wapate kushughulikia ujenzi mkubwa sana ambao kwa sasa wanamalizia kwa ajili ya Audio recording,Video production na Sehemu ya duka la nguo za jinsia zote pamoja na upambwaji wa vipodozi (cosmetics)
Akasema kwamba maboresho yanahusisha pia upande wa vifaa vya kurekodia kwani kuna vyombo vya studio alivyoagiza ambavyo kwa sasa vipo njiani toka kwenye tawi lao kubwa nchini Sweden kwa ajili ya Ubora zaidi wa Midundo na kuwezesha pia Urekodi wa Kikundi kama Kwaya au Bendi za Dance kwa wakati mmoja.
Akasisitiza kuwa ni ''vema vijana wakaheshimu na kutumia vizuri nafasi wanazopewa kwenye recording labels kwani uwekezaji wake ni mkubwa,na hakuna mafanikio yanayokuja kwa haraka kwani hapo awali tumejaribu kuwapa nafasi vijana toka sehemu tofauti lakini wamekuwa na tabia sizo kiasi kinachopelekea kukosa moyo na kudhani wote wapo hivyo kitu kinachopelekea kuogopa kuendelea na watu wa label..''Unajua sisi tangu kuanza kwetu shughuli hizi tumekuwa tukihangaika zaidi kuwatoa wasanii wachanga na pia kurudisha wasanii wakongwe ambao wapo tayari kwa hilo huu ndiyo mlengo wetu mkuu lakini sasa wanatulazimisha kutengenezeana mikataba migumu ya kimaandishi.
Akasisitiza kwa sasa hapokei label mpaka hapo studio itakapotangaza rasmi,ila anawasanii wawili ambao ni Big Born 90 chipukizi toka Chemba Squad na Mwana Hip Hop anaechukua Stashahada ya biashara ajulikanaye kama Famous-Champion.
Tunakaribisha mtu yeyote kufanya kazi kwa gharama zake pindi tutakapoanza toa huduma
.
PRODUCER DASH TOUCHEZ NAE ANENA.
Kwa upande wake muandaaji wa mziki dash-touchez anasisitiza kwamba bado hajatoa zile kazi ambazo zipo kabatini hivyo kama ni msanii jaribu kufanya ubunifu wa kuwa na mtindo wa kipekee ili uvutie mashabiki zako kwa midundo motomoto toka mikononi mwake.
Pia anawaasa wasanii kuzungumzia sehemu na watayarishaji waliohusika kuwaandalia kazi kwani wengi wao wamekuwa wakikaa kimya kwenye interviews kitu kinachoboa si kwa offisi ila hata kwake yeye kama muandaaji wa Mziki.
MSANII TOKA CHEMBA SQUAD BIG BORN 90
Mkali anaesumbua na wimbo wenye audio na video kali toka kwa muandaaji moe kaali aliye na kampuni One4pixel ujulikanao kama Mama Afrika,amesema mashabiki watarajie ngoma kali zitakazohusisha ujumbe maridhawa kulingana na maisha halisi yaliyotuzunguka kamwe hakuna katuni kwenye tungo zake. Pia akasisitiza upendo na amani miongoni mwa wasanii kwani hakuna maendeleo yanayoletwa na bifu.

MTAYARISHAJI WA MZIKI TOKA BIORN DASH-TOUCHEZ NA MKURUGENZI MOO G.
MTANGAZAJI WA RADIO RAS FM 100.3 DJ JADU TOKA DODOMA-TANZANIA
MAFUNDI UJENZI WAKIWA MZIGONI KUHAKIKISHA KILA KITU KINAKUWA SAWA
MKURUGENZI MOO G.(Mwenye kaoshi) AKISIMAMIA UJENZI IPASAVYO BIORN PROD.
LE SELFIE TOKA KWA BIG BORN 90,PRODUCER DASH-TOUCHEZ NA DIR. MOO G.
MKURUGENZI WA BIORN,MOO G. AKIWA NA MSANII FAMOUS CHAMPION & DOGO
MKURUGENZI WA BIORN DODOMA NA MTAYARISHAJI WA MUZIKI DASH TOUCHEZ.
SEHEMU YA JENGO LA STUDIO YA BIORN PRODUCTION UJENZI UKIENDELEA
No comments:
Post a Comment