Friday, April 3, 2015

MGAHAWA mkubwa unaotoa huduma za chakula cha Kitanzania unaomilikiwa na mpishi maarufu duniani, Issa Kapande `Chef Issa’, umefunguliwa nchini Sweden na kuvunja rekodi ya dunia.Mgahawa huo ulizinduliwa na balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu. Balozi Msechu alimpongeza Issa Kapande na mkewe kwa kufanikisha kuwapo kwa mgahawa huo ambao umeweka rekodi kuwa mgahawa mkubwa kuliko yote ya Kiafrika katika nchi za Ulaya. Aidha, alimshukuru Torvald Brahm mwenyeji wa mji huo kwa kumuunga mkono Issa hadi kufanikisha ndoto yake ya kuwa na mgahawa wa kwanza wa Kiafrika katika mji wa Trollhattan utakatoa huduma ya chakula cha kitanzania. Katika uzinduzi huo ambapo wenyeji wa manispaa hiyo akiwemo Meya na mwenyekiti wa Trollhattan, Paul Akerlund na msaidizi wake Peter Eriksson walikuwepo.Ndani ya mgahawa huo pia watu mbalimbali watapatiwa taarifa za utalii Tanzania. Katika kazi yake ya upishi, amebahatika kuwapikia watu mashuhuri duniani, baadhi wakiwa Andrew Young, Mchungaji Jesse Jackson, Robert Mugabe (Rais wa Zimbabwe), Paul Kagame (Rais wa Rwanda), Benjamini Mkapa (Rais mstaafu wa Tanzania), Raila Odinga (Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya), Daniel Arap Moi (Rais Mstaafu wa Kenya), Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bi. Hillary Clinton na mumewe Bill Clinton, Mke wa Rais wa zamani wa Marekani Laura Bush. Wengine ni Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, mwigizaji Chris Tucker, Rais wa zamani wa Afrika Kusini hayati Mzee Nelson Mandela, Koffie Olomide, Youssour ndour, Arsene Wenger (Kocha wa Arsenal ya England), Gianluca Vialli (nyota wa zamani wa Italia aliyewahi kuichezea na kuinoa Chelsea ya England), Rais wa Congo DRC, Joseph Kabila, Billy Gates na wengine wengi.Alisema Issa ameonesha njia kwamba inawezekana kwa watu waliopo Ughaibuni sio tu kuajiriwa, bali kujiajiri katika nyanja mbalimbali. Alisema hilo linawezekana kutokana na kufuatilia kwa karibu taratibu za wenyeji na kisha kutumia mafunzo yaliyopo kukamilisha ndoto. "Ni dhahiri kuwa, Chef Issa kwa kupitia taaluma yake ya upishi amewezeshwa kumiliki mgahawa huu hapa Trollhattan,S weden kwa hilo, napenda tuishangilie na kuipigia makofi Sweden na Trollhattan." Alisema akimpongeza kijana huyo ambaye pia amewekeza mkoani Mtwara. Katika mahojiano, Mpishi Mkuu Issa Kapande alisema mafanikio yake yanatokana na juhudi kubwa na nia aliyoiweka katika kujifunza na kufundisha wengine katika mitandao ya wapishi wakuu.

 Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu (wa tatu kushoto) akiwa na mwenyeji wake Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund (wa tatu kulia), Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania, Tagie Daisy Mwakawago (kulia), Mmiliki wa mgahawa unaotoa huduma za chakula cha kitanzania unaofahamika kama "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food) uliopo katika mji wa Trollhattan, Sweden unaomilikiwa na mtanzania Chef Issa Kapande (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na wadau mara baada ya kuwasili kwenye mnuso wa uzinduzi wa mgahawa huo

   Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu akiwa na mwenyeji wake Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund (kushoto) pamoja na Chef Issa Kapande (kulia) wakielekea kwenye eneo la tukio.
    WAGENI WAALIKWA WAKIENDELEA KUCHATI HUKU WAKISUBIRIA MAAKULI
    SEHEMU YA WAGENI WAALIKWA AMBAO NI WATANZANIA WAISHIO SWEDEN
   MMILIKI WA MGAHAWA HUO AKIONGEA KWA KUWAFAHAMISHA WAGENI ZAIDI
    MUHESHIMIWA BALOZI WA TANZANIA NCHI ZA SCANDNAVIA AKIPAKUA MSOSI
    MGENI AKIHUDUMIWA NA MMOJA WA WAFANYAKAZI WA HOTELI HIYO
   PICHA YA PAMOJA WAFANYAKAZI,MEYA WA MJI,BALOZI WETU NA MMILIKI

Mgahawa huo ulizinduliwa na balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu.
Balozi Msechu alimpongeza Issa Kapande na mkewe kwa kufanikisha kuwapo kwa mgahawa huo ambao umeweka rekodi kuwa mgahawa mkubwa kuliko yote ya Kiafrika katika nchi za Ulaya.

Aidha, alimshukuru Torvald Brahm mwenyeji wa mji huo kwa kumuunga mkono Issa hadi kufanikisha ndoto yake ya kuwa na mgahawa wa kwanza wa Kiafrika katika mji wa Trollhattan utakatoa huduma ya chakula cha kitanzania.

Katika uzinduzi huo ambapo wenyeji wa manispaa hiyo akiwemo Meya na mwenyekiti wa Trollhattan, Paul Akerlund na msaidizi wake Peter Eriksson walikuwepo

No comments:

Post a Comment