Sunday, May 17, 2015

MSANII BREEZY A.K.A. BABA LAO AMEFANYA INTERVIEW NA KITUO CHA TELEVISION CHA STAR TV JIJINI D'SALAAM NA KUTAMBULISHA VIDEO YAKE MPYA IJULIKANAYO KAMA ''MAMA LAO''

Msanii ajulikanaye kwa jina la Breezy a.k.a. baba lao kutoka mkoa husioishiwa vipaji uliopo katikati ya nchi ya Tanzania...Central Zone,,Dodoma wiki iliyopita ameachia rasmi video ya wimbo aliomshirikisha Msanii mwingine Malisam ujulikanao kama Mama Lao.
Video hiyo ameifanya kupitia Muongozaji Eris Mzava,imefanyika jijini Dar es salaam lakini Audio ya wimbo huo ilifanyika Dodoma chini ya Producer ama Mtayarishaji wa nyimbo kijana kuliko wote Kimambo Touchez.
Hivyo amefanikiwa kuafanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Star Tv,kipindi ambacho kitaenda hewani wiki hii muda wowote lakini tutakujuza kupitia kurasa zetu za mitandao hii ya kijamii kwani kitaenda live moja kwa moja toka jijini Dar es salaaa,Tanzania.
Amesema anashukuru wadau na uongozi wake kwani video yake ya Mama lao imepokelewa vizuri na jamii ama hadhara ya wadau wa soko la muziki na imempa imani kuwa itamfikisha mbali zaidi.
Alipoulizwa kuwa anawaahidi kipi mashabiki zake baaada ya hii kazi kwakuwa na mwanzo mzuri hakusita na kujibu ya kwamba watarajie ngoma nyingine kali siku za mbeleni kwani keshaifanya chini ya Producer na muimbaji Mensen Selector anaefanya shughuli zake chini kampuni ijulikanyo kwa jina la Defatality Music.
   Msanii breezy a.k.a Baba lao akiwa ndani ya ofisi za Star Tv kwa ajili ya Mahojiano ya kipindi

No comments:

Post a Comment