Thursday, May 14, 2015

USHAISKIA NGOMA HII KALI YENYE UJIO MPYA NA HISTORIA TOKA KWA WASANII WAKONGWE KWENYE GAME DODOMA(MAZICH REALITY) WAMEMSHIRIKISHA ONE SIX. MAZICH REALITY kama kundi lilianzishwa mnamo mwaka 1996 ikiwa ni muungano wa makundi mawili, DOGGDAZ PEACE MOB (DPM) na AFROU DOGZ (Ma-Mentali). Tukianza kutoka kundi la DPM liliwakilishwa na Mecky Mgonela a.k.a Ally Mzich akiwa na HAMDAN KIBWANA (R.I.P) a.k.a H. DAN. MEGSON NGAYOMOKA a.k.a MEGSOW na RAMADHAN TONADO waliwakilisha Kutoka upande wa AFROU DOGZ. Mnamo mwaka 1998 akaongezeka mwanakundi mwingine IBRAHIM SONA a.k.a King IBRAH. Mwaka 1999 mwanakundi mmoja aliyeitwa RAMSO alijiengua kwa ajili ya masomo; na hivyo kundi likabaki na wanakundi wanne tu. MAFANIKO Mwaka 1996 ulikuwa mwaka wake wa kwanza tangu kundi lianzishwe na lilifanikiwa kuchukua ubingwa mkoa wa Dodoma kwenye shindano lililofahamika wakati ule kama DODOMA RAP BONANZA. Kundi lilipata nafasi ya kuuwakilisha mkoa katika shindano la Ngazi ya Kitaifa ambalo hata hivyo halikufanyika. Kundi lilifanikiwa kupata mikataba mbalimbali ukiwamo mkataba na shirika la AFNET lililokuwa likishughulika na upigaji vita Ukeketaji na Unyanyasaji wa Kijinsia -- likiwa kama balozi kwa kanda ya kati. PIGO Mwaka 2000 kundi lilipata pigo baada ya kuondokewa na mwanachama mmoja (IBRA) aliyefariki dunia kwa ajali ya gari akiwa safarini Mtwara (Tutakukumbuka Daima King Ibrah) na basi kundi kubakia na watu watatu H. DAN MEGSAW ALEE MZICH PIGO TENA Mwaka 2002 kundi lilipata pigo tena kwa kuondokewa na mwanakundi mwingine (H. DAN) aliyefariki kwa maradhi ya Sickle Cell Anaemia yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu. Basi kundi likabakia na wanakundi wawili MEGSAW ALEE MZICH (Tutakukumbuka daima H. DAN) PIGO JINGINE Mwaka 2003 kundi llipata pigo jingine kwa kuondokewa na mwanakundi mwingine (RON) aliyefariki kwa ajali ya Piki Piki eneo la Nkuhungu, Dodoma. (Tutakukumbuka Daima RON) UJIO MPYA Baada ya wanakundi kufanya kazi mbalimbali wakiwa nje ya kundi, hatimaye kundi limerudi kufanya kazi likiwa na lengo la kufanya Albamu yao ya kwanza kama kundi. Katika kufanya hivyo kundi limetanguliza wimbo mmoja unaokwenda kwa jina la "Nimedata Nawe" -- likiwa limemshirikisha mkali wa viitikio anayekuja kwa kasi Afrika Mashariki; anayejulikana kwa jina la VICTOR a.k.a ONE SIX. Wimbo uliofanywa katika studio za AJ Records chini ya Mtayarishaji ABUU MTONI. Shukrani kwa Abuu Mtoni na AJ RECORDS." Salaam kwa Washabiki Wetu Wote ndani ya mkoa wa Dodoma ... Tuzidi kuwa pamoja na kuinua jukwaa letu la Burudani na Sanaa... Washabiki wetu na nje ya mkoa wa Dodoma. ... Popote mlipo tupo pamoja. Tunawapenda Wote Tukutane: www.facebook.com/mazichreality mazichreality@gmail.com


No comments:

Post a Comment