Thursday, May 21, 2015

MWANADADA MUIGIZAJI WA FILAMU ZA KITANZANIA AMBAYE PIA NI MLIMBWENDE ANAYEFANYA KAZI NA WASANII WA MUZIKI KWENYE PICHA ZA KUTEMBEA ( VIDEO QUEEN) ''RACHEL NJINGO'' ANAENDELEA KUSAMBAZA COPY ZA FILAMU YA CLARITHA IKIWEMO KUFANYA INTERVIEWS MEDIAS TOFAUTI

Msanii wa maigizo na Video queen 'Rachel Njingo' kutoka mkoani Dodoma nchini Tanzania,ameendelea kushukuru kwa sapoti ambayo jamii imeonyesha kwa kuipokea kazi yao kwa mikono miwili ambayo inajulikana kama Claritha.
Filamu hii ambayo ndiyo kwanza imekuwa ikisambaa mikoa toauti ya nchi yetu imeshampatia mahojiano (Interviews) kwenye vituo tofauti ndani na nje ya mkoa.
Mwana dada huyu ambae amekuwa akionekana pia kwenye vichupa (Videos) za wasanii tofauti ambao wanaimba bongo fleva,anasema kikubwa ni kuipenda kazi ufanyayo kwa moyo wote na kuzingatia ubora.
Hivi karibuni alikuwa mbeya kwa ajili ya usambazaji wa filamu hiyo,na baadae alielekea Mwanza ambapo pia alifanikiwa kufanya mahojiano na kituo kimojawapo cha radio metro fm  alishukuru watu wa mkoa huu uliopo kanda ya ziwa viktoria kwa kuwaambia...''Shukrani zangu za dhati kwa wakazi wa mwanza kutambua uwepo wangu natumai nakitukikubwa kwaajili yashukran kuileta nyumban shukran kwa media zote kussuport claritha ............kweli kizuri hutunzwa nyumban tegemeen heshima I love u mwanzaaa''
Rachel Njingo a.k.a. Super model unaweza ukamuona kwenye video ya msanii toka Dodoma 'Big born90-king' wimbo ambao amevaa uhusika wa Mama Afrika.
Ambao ulitayarishwa ndani ya Studio za biorn production tawi la dodoma chini ya producer Dash Touchez na Kufanyiwa video ya Kiwango cha juu na dairekta Moe Kaali wa One4 pixel production pia ni Muongozaji mwenye makazi mkoani dodoma.
Yupo pia kwenye video nyinginezo za wasanii ambao pia mashuhuri wa mziki wetu wa bongo fleva.

                              RECHO AKIWA KWENYE MAHOJIANO METRO FM JIJINI MWANZA
     SUPER MODEL RECHO AKIPOZI NA MWIGIZAJI GWIJI WA BONGO MOVIE JACK WOLPER
                          RECHO AKIWA KWENYE POZI MOJAWAPO KWA AJILI YA PICHA


  BAADHI YA FILAMU AMBAZO AMEWAHI KUSHIRIKI ZIKIWA SOKONI NDANI YA DUKA LA G-MOVIES LILILOPO MKOANI DODOMA
AKIPOZI NA WATANGAZAJI WA RADIO YA IMPACT FM MARA BAADA YA KUMALIZA INTERVIEW


 TEAM MVEME IKITOA USHIRIKIANO WA KUTOSHA KWENYE FILAMU YA CLARITHA IFIKIE RAIA
                     RACHEL NJINGO A.K.A. RSUPERMODEL AKIWA KWENYE POZI LA PICHA
   

No comments:

Post a Comment