Saturday, May 23, 2015

WASANII KUTOKA NCHINI CHILE WAFANYA COLABO NA MSANII WA BONGO MWENYE MAKAZI NCHINI SWEDEN ''KABOKU TANZANIANO''

Msanii wa kitanzania mwenye makazi yake nchini Sweden, ajulikanaye kwa jina la Kaboku Tanzaniano amerekodi wimbo kwa kuwashirikisha wasanii wawili toka nchini Chile Marques na nduguye,
Akizungumzia ngoma hiyo msanii huyo mwenye asili ya kundi la kaole jijini dar es salaam ambae ni mwenyeji wa kijitonyama mitaa ya block 41, amesema kwamba yeye anaishi kwa kufuata imani za ki-rasta hivyo upendo ni nguzo kubwa sana kwake,kupitia sanaa ya mziki yupo tayari kufanya colabo na mtu yeyote bila kujali anatokea upande upi wa Dunia.
Hivyo kwake imekuwa rahisi kufanya colabo na watu toka mataifa mbali mbali na ikizingatiwa yeye ni mtu mwenye uraia wa nje pia ya Tanzania hivyo anatumia nafasi hiyo kutangaza nchi mbili zote ambazo ameridhia kukaa.
Ameongeza kuwa anatarajia pia kuachia colabo itakayo mshirikisha msanii mmoja wa kike mkali sana toka pande za East afrika na kaishia kubashiri kwamba kama si Kenya huenda ikawa Uganda ambapo video yake inatarajiwa kuwa kali zadi toka kwa Mtayarishaji mahiri toka area code +256....ajulikanaye kwa jina la Bris De Ospinax.

No comments:

Post a Comment