Wednesday, May 27, 2015

KUTANA NA MKALI HUYU TOKA PANDE ZA DODOMA AMBAYE AMEKUBALI KUICHAMBUA HIP-HOP AKIWA UGHAIBUNI-SWEDEN

Katika kuhakikisha kwamba tunajifunza kile kilicho bora kwa manufaa ya jamii iliyotuzunguka,mkali huyu toka pande za Dom town ameamua kufunua vitabu vinavyoizungumzia sanaa ya muziki wa kufoka ( Hip Hop) kwa ajili ya kupata ufahamu zaidi ambao atautumia kwa kuwaelimisha wasanii wachanga ambao watakuwa tayari kupata msasa kupitia academy ya Mziki inayotarajiwa kuwepo siku za usoni kupitia tawi la Biorn production studios lililopo dodoma,Tanzania.
Akizungumza na mtandao huu moja kwa moja toka,jijini gothenburg-sweden,amesema dunia imekuwa kijiji kufuatana na teknolojia iliyopo hivyo inawezekana tukaelimishana bila kujali umbali tuliopo kati yetu.
Mchambuzi huyo Respicious Byonyu,anasisitiza vijana kujifunza au kupenda kuwa na elimu kwa kila jambo ambalo wanalifanya kwa mapenzi yao binafsi ili kuwa na uelewa mkubwa ambao utaongeza ufanisi.



No comments:

Post a Comment