Tuesday, May 26, 2015

KIMYA KINGI KINA MSHINDO MKUU - NI MANENO YA LE SUPER DIRECTOR DIR. ERICK BACKAMAZA II NA UJIO MPYA KABISA

Kama umewahi kuwa mpenzi wa videos za nyimbo za wasanii wa bongo fleva hususani wanaotokea pande za katikati ya nchi,iliyobarikiwa kila aina ya mali asili-Tanzania mkoa wa dodoma basi jina la Mtayarishaji na muongozaji wa picha za kutembea Erick Backamaza kamwe halitokuwa geni masikioni mwako.
Mkali huyu panapo tasnia hii ya video, amesema na kufunguka ya kwamba amekuwa kimya kwa kipindi fulani hapa kati na kuwa kwenye mazingira ya kutoachia kazi za kufuatana kama ilivyo ada, kwasababu alikuwa anajaribu kuweka sawa tu baadhi ya mambo ambayo yataboresha zaidi shughuli afanyazo,kupitia page hii amehakikisha anafikisha salamu kwa wapenzi wote wa burudani ya mziki wanaopenda kazi nzuri machoni mwao kwamba wakae tayari kupokea video zenye ubora na ubunifu wa hali ya juu kuazia mwezi ujao ambapo ametoa baaadhi tu ya picha zinazotarajiwa kuwepo kwenye kichupa kitakacho achiwa kama sehemu ya kufungulia pazia kazi mfululizo toka kwa wasanii tofauti ndani ya Tanzania na nje pia kulingana na nafasi au fursa zitakazo jitokeza kwani kuvuka borders nalo ni lengo kuu ili sanaa iwafikie walio wengi na kwa wakati.
Uongozi wa biorn production unaendelea kumpongeza na kumtakia mafanikio mema kupitia kazi azifanyazo kwa mikono yake,kwani amesaidia sana kuitangaza nyimbo iliyofanyika chini ya studio zetu zilizopo tawi la dodoma,aliyoimba mkali wa sauti hasiye na mpinzani kanda ya kati..msanii One six-victor ijulikanayo kwa jina la Maya.
Mungu ibariki,dodoma,tanzania,afrika na dunia kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment