Thursday, May 28, 2015

MSANII WA FILAMU WA KIKE AMBAYE PIA HUFANYA ULIMBWENDE KWENYE VIDEO ZA WAIMBAJI WA BONGO FLEVA..AMEITENDEA HAKI NYIMBO YA ''PNC'' KWA KUVAA UHUSIKA IPASAVYO

Kwa mara nyingine tena binti ajulikanaye kwa jina la Recho Njingo a.k.a. Rsupermodel,ameshirikishwa kwenye video ya msanii mkali wa miondoko ya bongo fleva Pnc na kuvaa uhusika kwa kiwango cha juu na kudhihirisha kwamba ameiva vya kutosha panapo tasnia hii ya video queen.
Kupitia wimbo huo ujulikanao kwa jina la yule yule, mwana dada huyu ameigiza kana kwamba alikuwa na mahusiano na mwimbaji Pnc lakini ikatokea hali ya kutoelewana na kupelekea msanii pnc kuchukua mkondo wa mahusiano kwa binti mwengine na hapo ndipo utamu wa kazi aifanyayo Recho ulipo.
Angalia video kamili kupitia link hiyo hapo chini hakika utakubali ya kwamba,mwana dada huyu ni moto wa kuotea mbali kwa kuigiza.
Endapo utakuwa umevutiwa na ufanyaji kazi wake kwenye Videos,unaweza kuwasiliana nasi kupitia pages zetu za Biorn production studios na tutakuunganisha na muhusika kwa ajili ya kazi.

https://www.youtube.com/watch?v=JFyiNzG8OOI


No comments:

Post a Comment