Sunday, May 31, 2015

MWANZA MWANZA MWANZA!!!!! DABO MTANZANIA + WAKAZI MUSIC + LADY JAYDEE WEEKEND INAMALIZIKIA HAPO

Team predator (Dabo Mtanzania) akishirikiana na wasanii wawili wa ziada ambao ni Wakazi music na Dada mkubwa Lady Jaydee weekend hii wanaendelea kuwasha moto Kanda ya ziwa jijini Mwanza a.k.a. Rock City.
Shughuli nzima ilianzia jana pande za Geita kwenye ukumbi wa Desire Park,wakali hawa walishambulia stage na kufanya shangwe zitawale kila kona japo mvua ilileta vurugu zake kiasi fulani.
Leo jpili usiku huu kuna happen show yao nyingine ya nguvu Mwanza mjini ndani ya sehemu tulivu ijulikanayo kwa jina la ''Isamilo'' kama upo pande hizo si ya kukosa kwani wakali watatu ndani ya Jukwaa moja ni kitu kikubwa kwenye burudani ya mziki wetu wa nyumbani na ni nafasi pekee Ambayo hutokea kwa nadra.
Pia usisahau kuwapigia kura kwenye tuzo za mziki za Kilimanjaro music awards ili waweze kushinda tuzo ya wimbo bora wa kushirikiana.. .Jaydee Ft: Dabo wimbo ''Forever'' sms AL 1 kwenda namba 15415
Au tuma KILI au KTMA..chagua A: wimbo namba 30 kisha andika code AL 1 kupitia www.kilitime.co.tz/ktma.
Tusapoti mziki mzuri kumbuka tumebakiwa na wiki mbili tu.

No comments:

Post a Comment