Thursday, July 9, 2015

DANCERS TOKA BIORN PRODUCTION WAJULIKANAO KAMA ''THE WINNERS'' WASHINDA KWENDA KUIWAKILISHA TANZANIA NJE YA NCHI MICHUANO YA NTV NAIROBI IJULIKANAYO KAMA ''SAKATA DANCE''

Kikundi cha vijana wa dancing kinachomilikiwa na kampuni ya Biorn Production kimeendelea kufanya vema kwenye mashindano ya aina mbali mbali yanayoendeshwa na wadau wa aina tofauti ndani na nje ya nchi.
Kikundi hiki kinachoendelea kujizolea umaarufu kila kukicha kijulikanacho kama the winners team biorn kimeshiriki michuano ya Sakata dance iliyoandaliwa na kituo cha televisheni nchini kenya jijini Nairobi ( Ntv) na kufanikwa kujinyakulia ushindi wa kwenda kwenye fainali za kuiwakilisha nchi ya Tanzania zitakazo husisha mataifa matano ya nchi jirani za afrika ya mashariki.
Mchujo wa kuelekea nchini Kenya kwenye fainali hizo ulifanyika kitaifa pale Don Bosco upanga jijini Dar es salaam na kuhusisha vikundi themanini na tatu (83) toka pembe mbali mbali za nchi na kuchukua washindi watano kwa kuliwakilisha taifa nje ya nchi.
Kwa sasa taratibu zote za awali zilishakamilika hivyo vijana wanasubiria hati zao za kusafiria toka idara ya uhamiaji (pasports)
Fainali hizo za Sakata Dance zinatarajia kufanyanyika siku za hivi karibuni ndani ya jiji la Nairobi,zikihusisha mataifa yote matano ya nchi za Afrika ya mashariki ambapo waandaaji wakuu ni Ntv ya Kenya,inatarijiwa kuwa na patashika kubwa kwani vikundi vyote ni vikali hivyo imeleta msisimko mkubwa kwenye haya mashindano.


No comments:

Post a Comment